Isaiah 54:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakuita urudi kana kwamba ulikuwa mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni; kama mke aliyeolewa bado angali kijana na kukataliwa,” asema Mungu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Yerusalemu, Mwenyezi-Mungu amekuita tena wewe kama vile mke aliyeachwa na kuhuzunika, mke aliyeolewa akiwa kijana akaachwa. Mungu wako anasema:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ulipokuwa mwanamke aliyeachwa, aliyesikitika rohoni, Bwana alikuita. Naye mke wa ujana anakataliwaje? Ndivyo, Mungu wako anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA amekuita kama mke aliyeachwa na kuhuzunishwa rohoni, kama mke wakati wa ujana, atupwapo, asema Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yerusalema, Yawe amekuita tena. Ulikuwa kama vile muke aliyeachwa na kuhuzunika. Mungu wako anasema: Muke aliyeolewa akiwa kijana, anaweza kuachiliwa?