Isaiah 54:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuonea huruma. Mimi Mwenyezi-Mungu Mkombozi wako, nimesema.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika ukali wa hasira nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuwa na huruma juu yako,” asema Mwenyezi Mungu Mkombozi wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuonea huruma. Mimi Mwenyezi-Mungu Mkombozi wako, nimesema.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika ukali wa hasira nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuwa na huruma juu yako,” asema BWANA Mkombozi wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika ukali wa hasira nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuwa na huruma juu yako,” asema bwana Mkombozi wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa ghadhabu ifurikayo nilikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuonea huruma. Mimi Mwenyezi-Mungu Mkombozi wako, nimesema.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makali yalipofurika, nimeuficha uso wangu punde kidogo, usiuone, lakini kwa upole ulio wa kale na kale nitakuhurumia; ndivyo, Bwana aliye mkombozi wako anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hasira nyingi nilikuficha uso wangu kwa muda kidogo, lakini kwa wema wa milele nitakuonea huruma. Ni Yawe Mukombozi wako anayesema hivyo.