Isaiah 55:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Badala ya michongoma kutamea misonobari, na badala ya mbigili kutamea mihadasi. Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu juu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu; ishara ya milele ambayo haitafutwa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala ya kichaka cha miiba itaota miti ya misunobari, na badala ya michongoma utaota mhadasi. Hili litakuwa jambo la kumpatia Mwenyezi Mungu jina, kwa ajili ya ishara ya milele, ambayo haitaharibiwa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Badala ya michongoma kutamea misonobari, na badala ya mbigili kutamea mihadasi. Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu juu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu; ishara ya milele ambayo haitafutwa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala ya kichaka cha miiba itaota miti ya misunobari, na badala ya michongoma utaota mhadasi. Hili litakuwa jambo la kumpatia BWANA jina, kwa ajili ya ishara ya milele, ambayo haitaharibiwa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala ya kichaka cha miiba itaota miti ya misunobari, na badala ya michongoma utaota mhadasi. Hili litakuwa jambo la kumpatia bwana jina, kwa ajili ya ishara ya milele, ambayo haitaharibiwa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Badala ya michongoma utamea msonobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Badala ya michongoma kutamea misonobari, na badala ya mbigili kutamea mihadasi. Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu juu ya mambo niliyotenda mimi Mwenyezi-Mungu; ishara ya milele ambayo haitafutwa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Palipokuwa na mikunju tu, patakuwa na mivinje, napo palipokuwa na viwawi tu, patakuwa na miti ya vihagilo, nayo miti hiyo italitangaza Jina la Bwana, iwe kielekezo chake cha kale na kale kisichong'oleka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia BWANA jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pahali pa miiba kutaota miti ya shindano, na pahali pa michongoma kutaota misunobari. Hilo litakuwa jambo litakalowakumbusha watu juu ya mambo niliyotenda mimi Yawe, kitambulisho cha milele ambacho hakitafutwa.