Isaiah 56:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu. Maana nyumba yangu itaitwa: ‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu. Maana nyumba yangu itaitwa: ‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu, kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
hawa nitawaleta kwenye mlima wangu mtakatifu na kuwapa furaha ndani ya nyumba yangu ya sala. Sadaka zao za kuteketeza na dhabihu zao zitakubalika juu ya madhabahu yangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitawaleta hao nao hadi katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
hao nitawaleta katika mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; tambiko na sadaka zao zitakubaliwa madhabahuni pangu. Maana nyumba yangu itaitwa: ‘Nyumba ya sala kwa ajili ya watu wote’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
hawa nitawapeleka kwenye mlima wangu mtakatifu, niwafurahishe Nyumbani mwangu mwa kuombea, nazo ng'ombe zao za tambiko na vipaji vyao vingine vya tambiko vitanipendeza vitakapotolewa mezani pangu pa kunitambikia, kwani Nyumba yangu itaitwa nyumba ya kuombea kwao makabila yote ya watu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitawaleta hao nao hata mlima wangu mtakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya sala; makafara yao na dhabihu zao zitakubaliwa juu ya madhabahu zangu; kwa maana nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa mataifa yote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
hao nitawaleta katika mulima wangu mutakatifu, na kuwafurahisha katika nyumba yangu ya maombi; sadaka zao na sadaka za kuteketezwa zitakubaliwa kwenye mazabahu yangu. Maana nyumba yangu itaitwa: Nyumba ya maombi kwa ajili ya watu wote.