Isaiah 56:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana Mungu Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya na wengine kwao zaidi ya hao ambao wameshakusanywa tayari.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenyezi asema, yeye awakusanyaye Waisraeli waliohamishwa: “Bado nitawakusanya wengine kwao zaidi ya hao ambao wamekusanywa tayari.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Hii ni kauli yangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu ninayewakusanya Waisraeli waliotawanyika. Licha ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wajumuike nao.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, asemavyo Bwana Mungu anayewakusanya Waisiraeli waliotawanyika: Wako wengine wa kwao, nitakaowakusanya, niwatie kwao waliokusanywa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya hao walio wake waliokusanywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
–Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe, yule anayewakusanya Waisraeli waliosambazwa.– Zaidi ya hao niliokwisha kukusanya, nitawakusanya watu wengine wakutane nao.