Isaiah 57:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao; niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika. Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi; nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira, na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao; niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika. Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi; nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira, yeye bado aliendelea katika njia zake za tamaa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilighadhibika na tamaa yake ya dhambi; nilimwadhibu, nikauficha uso wangu kwa hasira, na bado aliendelea katika njia zake za tamaa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake niliona hasira, nikampiga; nilificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao; niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika. Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ubaya wa choyo chao niliukasirikia, nikawapiga nikijificha kwa kuwa na makali, nao wakajiendea na kuniacha, wakashika njia za kuipendeza mioyo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu ya uovu wa kutamani kwake naliona hasira, nikampiga; nalificha uso wangu, nikaona ghadhabu; naye akaendelea kwa ukaidi, kuifuata njia ya moyo wake mwenyewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao; niliwaazibu, nikauficha uso wangu na kukasirika. Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.