Isaiah 57:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnachagua mawe laini mabondeni, na kuyafanya kitovu cha maisha yenu. Mnayamiminia tambiko ya kinywaji na kuyapelekea tambiko ya nafaka! Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Sanamu zilizo kati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu; hizo ndizo sehemu yenu. Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji, na kutoa sadaka za nafaka. Katika haya yote, niendelee kuona huruma?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Sehemu yako i katika makokoto ya bonde; hayo ndiyo kura yako; umeyamwagia hayo sadaka ya kinywaji, umeyatolea sadaka ya unga; je! Niwe radhi na mambo hayo?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnachagua mawe laini mabondeni, na kuyafanya kitovu cha maisha yenu. Mnayamiminia tambiko ya kinywaji na kuyapelekea tambiko ya nafaka! Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Sanamu zilizoko katikati ya mawe laini ya mabondeni ndiyo fungu lenu; hizo ndizo sehemu yenu. Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji, na kutoa sadaka za nafaka. Kwa ajili ya haya yote, niendelee kuona huruma?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Sanamu zilizo katikati ya mawe laini ya mabondeni ndizo fungu lenu; hizo ndizo sehemu yenu. Naam, kwa hizo mmemimina sadaka za vinywaji, na kutoa sadaka za nafaka. Katika haya yote, niendelee kuona huruma?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Sehemu yako i katika makokoto ya bonde; hayo ndiyo kura yako; umeyamwagia hayo sadaka ya kinywaji, umeyatolea sadaka ya unga; je! Niwe radhi na mambo hayo?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnachagua mawe laini mabondeni, na kuyafanya kitovu cha maisha yenu. Mnayamiminia tambiko ya kinywaji na kuyapelekea tambiko ya nafaka! Je, mimi nitaridhishwa kwa vitu hivyo?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mawe ya mtoni yatelezayo na fungu lako, hayo ndiyo, unayoyatumia kuwa kura yako; nayo huyamwagia vinywaji vya tambiko, ukayatolea hata vilaji vya tambiko. Sasa je? Hayo niyanyamazie tu?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Sehemu yako i katika makokoto ya bonde; hayo ndiyo kura yako; umeyamwagia hayo sadaka ya kinywaji, umeyatolea sadaka ya unga; je! Niwe radhi na mambo hayo?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munachagua mawe laini katika mabonde, na kuyafanya kuwa mungu wenu. Munayamwangia sadaka ya kinywaji na kuyapelekea sadaka ya unga! Mimi nitatulizwa kwa vitu hivyo?