Isaiah 57:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyuma ya milango na miimo mmetundika kinyago chenu. Nyinyi mnaniacha mimi na kutandika na kuvipanua vitanda vyenu. Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao. Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya, huku mnakodolea macho kinyago chenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nyuma ya milango yako na miimo yako umeweka alama zako za kipagani. Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako, umepanda juu yake na kukipanua sana; ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao, nawe uliangalia uchi wao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyuma ya milango na miimo mmetundika kinyago chenu. Nyinyi mnaniacha mimi na kutandika na kuvipanua vitanda vyenu. Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao. Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya, huku mnakodolea macho kinyago chenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nyuma ya milango yako na miimo yako umeweka alama zako za kipagani. Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako, umepanda juu yake na kukipanua sana; ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao, nawe uliangalia uchi wao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nyuma ya milango yako na miimo yako umeweka alama zako za kipagani. Kwa kuniacha mimi, ulifunua kitanda chako, umepanda juu yake na kukipanua sana; ulifanya patano na wale ambao unapenda vitanda vyao, nawe uliangalia uchi wao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyuma ya milango na miimo mmetundika kinyago chenu. Nyinyi mnaniacha mimi na kutandika na kuvipanua vitanda vyenu. Mnafanya mapatano na hao mliopenda vitanda vyao. Humo mnazitosheleza tamaa zenu mbaya, huku mnakodolea macho kinyago chenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa kuniacha mimi unakiweka kinyago chako cha nyumbani nyuma ya mlango kwenye miimo; kisha ukakifunua kilalo chako, ukakipanda, ukakipanua, ukajichagulia mmoja wao, ukapenda kulala nao, ulipoona mkono uliokupungia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nyuma ya milango na miimo umeweka kumbukumbu lako; kwa maana umejifunua nafsi yako kwa ajili ya mwingine, si kwa ajili yangu, ukakwea juu; umekipanua kitanda chako, nawe umefanya maagano na hao; ulikipenda kitanda chao hapo ulipokiona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nyuma ya milango na miimo mumetundika sanamu yenu. Ninyi munaniacha mimi. Mumevua nguo zenu na kupanda juu ya vitanda vyenu vipana. Mumelipa wapenzi wenu ambao munataka kulala nao. Halafu munatimiza tamaa zenu mbaya.