Isaiah 57:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnajitia marashi na manukato kwa wingi kisha mnakwenda kumwabudu Moleki. Mnawatuma wajumbe wenu huko na huko, kujitafutia miungu ya kuabudu; hata kuzimu walifika.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ulienda kwa Moleki ukiwa na mafuta ya zeituni, na ukaongeza manukato yako. Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, ukashuka kwenye kaburi lenyewe!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnajitia marashi na manukato kwa wingi kisha mnakwenda kumwabudu Moleki. Mnawatuma wajumbe wenu huko na huko, kujitafutia miungu ya kuabudu; hata kuzimu walifika.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ulikwenda kwa Moleki ukiwa na mafuta ya zeituni na ukaongeza manukato yako. Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, ukashuka kwenye kaburi lenyewe!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ulikwenda kwa Moleki ukiwa na mafuta ya zeituni, na ukaongeza manukato yako. Ukawatuma wajumbe wako mbali sana, ukashuka kwenye kaburi lenyewe!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hadi kuzimu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnajitia marashi na manukato kwa wingi kisha mnakwenda kumwabudu Moleki. Mnawatuma wajumbe wenu huko na huko, kujitafutia miungu ya kuabudu; hata kuzimu walifika.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukasafiri kumwendea mfalme ukichukua mafuta ya kukipaka na manukato yako mengi, ukatuma wajumbe wako kwenda katika nchi za mbali, ukawaendesha hata kushuka kuzimuni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ulimwendea mfalme na mafuta ya marhamu, ukaongeza manukato yako, ukawatuma wajumbe wako waende mbali, ukajidhili sana hata kuzimu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munajipakaa marasi na mafuta kwa wingi kisha munakwenda kumwabudu Moleki. Munawatuma wajumbe wenu huko na huko, kujitafutia miungu ya kuabudu; hata kuzimu walifika.