Isaiah 58:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa, mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki, mwanga utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama mchana.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
nanyi mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu na kutosheleza mahitaji ya waliodhulumiwa, ndipo nuru yenu itang’aa gizani, nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa, mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki, mwanga utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama mchana.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu na kutosheleza mahitaji ya walioonewa, ndipo nuru yenu itakapong'aa gizani, nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
nanyi kama mkimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi zenu na kutosheleza mahitaji ya walioonewa, ndipo nuru yenu itakapong’aa gizani, nao usiku wenu utakuwa kama adhuhuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na kama ukimpa mtu mwenye njaa chakula chako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa, mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki, mwanga utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama mchana.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwenye njaa utakapompa, roho yako iyatakayo nayo, utakapoishibisha roho ya mkiwa, ndipo, mwanga wako utakapotokea gizani, ndipo, weusi wa usiku utakapokuwa kwako kama jua la mchana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na kama ukimkunjulia mtu mwenye njaa nafsi yako, na kuishibisha nafsi iliyoteswa; ndipo nuru yako itakapopambazuka gizani; na kiwi chako kitakuwa kama adhuhuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
mukiwapa wenye njaa chakula, mukitimiza mahitaji ya wenye kuteswa, mwangaza utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama muchana.