Isaiah 58:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji, kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayakauki kamwe.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakuongoza siku zote, atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame, naye ataitia nguvu mifupa yako. Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri, kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Naye Bwana atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji, kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayakauki kamwe.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakuongoza siku zote, atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame, naye ataitia nguvu mifupa yako. Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri, kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakuongoza siku zote, atayatosheleza mahitaji yako katika nchi kame, naye ataitia nguvu mifupa yako. Utakuwa kama bustani iliyonyweshwa vizuri, kama chemchemi ambayo maji yake hayakauki kamwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji, kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayakauki kamwe.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Naye Bwana atakuongoza siku zote, aishikize roho yako katika nchi kavu; nayo mifupa yako ataishupaza, uwe kama shamba lililonyweshwa au kama kisima cha maji kisichodanganya kwa kuwa na maji yasiyokauka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Naye BWANA atakuongoza daima, ataishibisha nafsi yako mahali pasipokuwa na maji, na kuitia nguvu mifupa yako; nawe utakuwa kama bustani iliyotiwa maji, na kama chemchemi ambayo maji yake hayapungui.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Yawe nitawaongoza siku zote, nitatimiza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha katika mwili, nanyi mutakuwa kama bustani iliyomwangiliwa maji, kama chemichemi ya maji ambayo maji yake hayakauki hata kidogo.