Isaiah 58:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Magofu yenu ya kale yatajengwa; mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani. Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta, watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu wako watajenga tena magofu ya zamani na kuinua misingi ya kale; utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka, Mwenye Kurejesha Barabara za Makao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Magofu yenu ya kale yatajengwa; mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani. Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta, watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu wako watajenga tena magofu ya zamani na kuinua misingi ya kale; utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka, Mwenye Kufanya upya Barabara zenye Makazi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu wako watajenga tena magofu ya zamani na kuinua misingi ya kale; utaitwa Mwenye Kukarabati Kuta Zilizobomoka, Mwenye Kurejeza Barabara za Makao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejesha njia za kukaa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Magofu yenu ya kale yatajengwa; mtajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani. Nanyi mtaitwa watu waliotengeneza upya kuta, watu waliozifanya barabara za mji zipitike tena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watakaotoka kwako watayajenga mabomoko yako ya kale, nayo misingi ya vizazi na vizazi utaitengeneza tena; kwa hiyo watakuita: Mjenga nyufa na Mfufua njia, watu wakae.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wako watapajenga mahali palipokuwa ukiwa; utaiinua misingi ya vizazi vingi; nawe utaitwa, Mwenye kutengeneza mahali palipobomoka; na, Mwenye kurejeza njia za kukalia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wako watajenga tena mabomoko ya zamani; mutajenga upya juu ya misingi iliyoachwa zamani. Nanyi mutaitwa watu waliotengeneza upya kuta, watu waliotengeneza tena barabara za miji.