Isaiah 58:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha; mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi, na kulalia nguo za magunia na majivu. Je, huo ndio mnaouita mfungo? Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua, siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza? Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete, na kwa kujilaza juu ya gunia na majivu? Je, huo ndio mnaouita mfungo, siku iliyokubalika kwa Mwenyezi Mungu?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na Bwana?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha; mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi, na kulalia nguo za magunia na majivu. Je, huo ndio mnaouita mfungo? Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua, siku moja tu kwa ajili ya mtu kujinyenyekeza? Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama unyasi Na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu? Je, huo ndio mnaouita mfungo, siku iliyokubalika kwa BWANA?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, hii ndiyo aina ya mfungo niliouchagua, siku moja tu ya mtu kujinyenyekeza? Je, ni kwa kuinamisha kichwa chini kama tete, na kwa kujilaza juu ya nguo ya gunia na majivu? Je, huo ndio mnaouita mfungo, siku iliyokubalika kwa bwana?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfungapo, nyinyi mnajitaabisha; mnaviinamisha vichwa vyenu kama unyasi, na kulalia nguo za magunia na majivu. Je, huo ndio mnaouita mfungo? Je, hiyo ni siku inayokubaliwa nami?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Huo ndio mfungo, nilioupenda, uwe siku, mtu anapojinyima yamfaayo? Mtu akikiinamisha kichwa chake kama unyasi, tena akilalia gunia na majivu,, huo utauita mfungo na siku ya kumpendeza Bwana?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Kufunga namna hii ni saumu niliyoichagua mimi? Je! Ni siku ya mtu kujitaabisha nafsi yake? Ni kuinama kichwa kama unyasi, na kutanda nguo za magunia na majivu chini yake? Je! Utasema ni siku ya kufunga, na ya kukubaliwa na BWANA?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munapofunga kula, ninyi munajitaabisha; munaviinamisha vichwa vyenu kama utete, na kulalia nguo za magunia na majivu. Hii ndio munayoita mafungo ya kula chakula? Hiyo ni siku inayonipendeza mimi?