Isaiah 58:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: Kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachia huru wanaokandamizwa, na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua: kufungua minyororo ya udhalimu, na kufungua kamba za nira, kuwaweka huru waliodhulumiwa, na kuvunja kila nira?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: Kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachia huru wanaokandamizwa, na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua: kufungua minyororo ya udhalimu na kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioonewa na kuvunja kila nira?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Je, hii si ndiyo aina ya mfungo niliyoichagua: kufungua minyororo ya udhalimu, na kufungua kamba za nira, kuwaweka huru walioonewa, na kuvunja kila nira?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: Kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachia huru wanaokandamizwa, na kuvunjilia mbali udhalimu wote!
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Je? Mfungo, nilioupenda sio huu: kufungua mafungo ya ukorofi, kulegeza kamba za utumwa, kuwapa ruhusa waliopondeka, wajiendee, kuvunja utumwa wo wote?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Saumu niliyoichagua, siyo ya namna hii? Kufungua vifungo vya uovu, kuzilegeza kamba za nira, kuwaacha huru walioonewa, na kwamba mvunje kila nira?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mafungo ninayotaka mimi ni haya: kuwafungua waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaacha huru wanaogandamizwa, na kuvunja kabisa mambo yote ya kitumwa!