Isaiah 58:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi, unapomwona aliye uchi, umvike, wala si kumkimbia mtu wa mwili wako na damu yako mwenyewe?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi, unapomwona aliye uchi, umvike, wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Je, sio kushirikiana chakula chako na wenye njaa na kuwapatia maskini wasiokuwa na makao hifadhi, unapomwona aliye uchi, umvike, wala si kumkimbia mtu wa nyama na damu yako mwenyewe?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usikose kumsaidia mtu aliye jamaa yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Sivyo hivyo? Ukimgawia mwenye njaa mkate wako. ukiingiza nyumbni mwako wakiwa waliofukuzwa, unapoona mwenye uchi ukimpa nguo, usipowakataa walio wa mlango wako?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Je! Siyo kuwagawia wenye njaa chakula chako, na kuwaleta maskini waliotupwa nje nyumbani kwako? Umwonapo mtu aliye uchi, umvike nguo; wala usijifiche na mtu mwenye damu moja nawe?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mafungo ya kweli ni kugawanya chakula chako pamoja na wenye njaa, kuwakaribisha katika nyumba yako wamasikini wasiokuwa na makao, kuwavalisha wasiokuwa na nguo, bila kusahau kuwasaidia wandugu zenu.