Isaiah 58:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa Mwenyezi Mungu utakuwa mlinzi nyuma yako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa Bwana utakufuata nyuma ukulinde.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mkifanya hivyo mtang'ara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa BWANA utakuwa mlinzi nyuma yako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ndipo nuru yako itajitokeza kama mapambazuko na uponyaji wako utatokea upesi; ndipo haki yako itakapokutangulia mbele yako, na utukufu wa bwana utakuwa mlinzi nyuma yako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na uponyaji wako utatokea punde; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mkifanya hivyo mtangara kama pambazuko, mkiwa wagonjwa mtapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalindeni kutoka nyuma kwa utukufu wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ukifanya hivyo, ndipo, mwanga wako utakapopambazuka kama mionzi ya jua, ndipo, vidonda vyako vitakapopona upesi, ndipo, wongofu wako utakapokutangulia, nao utukufu wa Bwana utakufuata nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo nuru yako itakapopambazuka kama asubuhi, na afya yako itatokea mara; na haki yako itakutangulia; utukufu wa BWANA utakufuata nyuma ukulinde.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mukifanya hivyo mutaonekana kama mwangaza wa mapambazuko, na mutapona haraka. Matendo yenu mema yatawatangulia, nami nitawalinda kutoka nyuma kwa utukufu wangu.