Isaiah 59:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama vipofu twapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasio na macho. Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku, miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tunapapasa ukuta kama vipofu, tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho. Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza; kati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Twapapasa-papasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao waliowanda tumekuwa kama wafu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama vipofu twapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasio na macho. Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku, miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tunapapasa ukuta kama kipofu, tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho. Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza, katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tunapapasa ukuta kama vipofu, tunapapasa katika njia zetu kama watu wasio na macho. Adhuhuri tunajikwaa kama wakati wa gizagiza; katikati ya wenye nguvu, tuko kama wafu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Twapapasapapasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao walionenepa tumekuwa kama wafu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama vipofu twapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasio na macho. Tunajikwaa mchana kana kwamba ni usiku, miongoni mwa wenye nguvu sisi ni kama wafu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tunapapasa ukutani kama vipofu, kweli tunapapasa tu kama watu wasio na macho; tunajikwaa na mchana, kama ni jioni, tuko kama wafu kwao walio wenye nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Twapapasa-papasa kutafuta ukuta kama kipofu, naam, twapapasa kama watu wasio na macho; twajikwaa wakati wa adhuhuri, kana kwamba ni wakati wa ukungu wa alfajiri; kati yao waliowanda tumekuwa kama wafu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vipofu tunapapasapapasa ukuta; tunasitasita kama watu wasiokuwa na macho. Tunajikwaa muchana kati, sawa vile ni usiku; kati ya wenye afya, sisi ni kama wafu.