Isaiah 59:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atawaadhibu maadui kadiri ya matendo yao, naam, ghadhabu yake na kisasi vitawapata maadui zake; atawaadhibu hata wakazi wa nchi za mbali.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kulingana na kile walichokuwa wametenda, ndivyo atakavyolipa ghadhabu kwa watesi wake na kisasi kwa adui zake, atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atawaadhibu maadui kadiri ya matendo yao, naam, ghadhabu yake na kisasi vitawapata maadui zake; atawaadhibu hata wakazi wa nchi za mbali.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kulingana na kile walichokuwa wametenda, ndivyo atakavyolipa ghadhabu kwa watesi wake na kisasi kwa adui zake, atavilipa tena visiwa sawa na wanavyostahili.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kulingana na kile walichokuwa wametenda, ndivyo atakavyolipa ghadhabu kwa watesi wake na kisasi kwa adui zake, atavilipa visiwa sawa na wanavyostahili.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri hiyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atawaadhibu maadui kadiri ya matendo yao, naam, ghadhabu yake na kisasi vitawapata maadui zake; atawaadhibu hata wakazi wa nchi za mbali.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama matendo yao yalivyo, ndivyo, nayo malipizi yatakavyokuwa: makali yatawatokea waliompingia, nao waliomchukia watafanyiziwa vivyo hivyo, hata visiwa atavilipisha matendo yao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kadiri ya matendo yao, kwa kadiri iyo hiyo atawalipa, ukali kwao wampingao, malipo kwa adui zake; naye atavirudishia visiwa malipo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Atawaazibu waadui kadiri ya matendo yao, kasirani yake na kisasi vitawapata waadui zake; atawaazibu hata wakaaji wa inchi za mbali.