Isaiah 59:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toka magharibi hadi mashariki, kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama mto uendao kasi, mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la Mwenyezi Mungu na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake. Adui atakapokuja kama mafuriko, Roho wa Mwenyezi Mungu atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, wataliogopa jina la Bwana toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toka magharibi hadi mashariki, kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama mto uendao kasi, mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la BWANA na kuanzia maawio ya jua, watauheshimu utukufu wake. Wakati adui atakapokuja kama mafuriko, Roho wa BWANA atainua kiwango dhidi yake na kumshinda kumfukuza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuanzia magharibi, watu wataliogopa jina la bwana na kuanzia mawio ya jua, watauheshimu utukufu wake. Wakati adui atakapokuja kama mafuriko, Roho wa bwana atainua kiwango dhidi yake na kumshinda.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka mawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toka magharibi hadi mashariki, kila mtu atamcha Mwenyezi-Mungu na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama mto uendao kasi, mto unaosukumwa kwa upepo wa Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, watakapoliogopa Jina la Bwana machweoni kwa jua, nako maawioni kwa jua watauogopa utukufu wake, kwani atakuja kama mto unaopita mahali pembamba, upepo wa Bwana ukiyasukuma maji yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, wataliogopa jina la BWANA toka magharibi, na utukufu wake toka maawio ya jua; maana yeye atakuja kama mkondo wa mto ufurikao, uendeshwao kwa pumzi ya BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Toka magaribi mpaka mashariki, kila mutu atamwogopa Yawe na kutambua utukufu wake. Maana atakuja kama muto wenye kuporomoka mbio, muto unaosukumwa kwa upepo wa Yawe.