Isaiah 59:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nafanya nanyi agano hili: Roho yangu niliyowajazeni, maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu, hayataondoka kwenu kamwe, wala kwa watoto na wajukuu zenu, tangu sasa na hata milele.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Bali mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema Mwenyezi Mungu. “Roho wangu Mtakatifu, aliye juu yenu, na maneno yangu niliyoyaweka vinywani vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema Bwana; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema Bwana, tangu leo na hata milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nafanya nanyi agano hili: Roho yangu niliyowajazeni, maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu, hayataondoka kwenu kamwe, wala kwa watoto na wajukuu zenu, tangu sasa na hata milele.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa habari yangu mimi, hili ni Agano langu nao,” asema BWANA. “Roho wangu, aliyeko juu yenu na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu hayataondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao kuanzia sasa na hata milele,” asema BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa habari yangu mimi, hili ndilo agano langu nao,” asema bwana. “Roho wangu, aliye juu yenu, na maneno yangu ambayo nimeyaweka katika vinywa vyenu, havitaondoka vinywani mwenu, wala kutoka vinywani mwa watoto wenu, wala kutoka vinywani mwa wazao wao, kuanzia sasa na hata milele,” asema bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena kuhusu habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu asema: “Mimi nafanya nanyi agano hili: Roho yangu niliyowajazeni, maneno niliyoyaweka mdomoni mwenu, hayataondoka kwenu kamwe, wala kwa watoto na wajukuu zenu, tangu sasa na hata milele.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivi ndivyo, Bwana anavyosema: Hili ni agano langu mimi, ninalolifanya nao: Roho yangu inayokukalia na maneno yangu, niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala vinywani mwao walio wa uzao wako, wala mwao walio uzao wa uzao wako, kuanzia sasa hata kale na kale; ndivyo, Bwana anavyosema.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena katika habari zangu, hili ndilo agano langu nao, asema BWANA; roho yangu iliyo juu yako, na maneno yangu niliyoyatia kinywani mwako, hayataondoka kinywani mwako, wala kinywani mwa wana wako, wala kinywani mwa wajukuu wako, asema BWANA, tangu leo na hata milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe anasema: Mimi ninafanya nanyi agano hili: Roho wangu anayekuwa juu yenu, maneno niliyoyaweka katika kinywa chenu, hayataondoka kwenu hata kidogo, wala kwa watoto na wajukuu wenu, tangu sasa na hata milele.