Isaiah 59:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hakuna atoaye madai yake kwa haki, wala anayeshtaki kwa uaminifu. Mnategemea hoja batili; mnasema uongo. Mnatunga hila na kuzaa uovu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki; hakuna hata mmoja anayetetea kwa haki. Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo, huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hakuna atoaye madai yake kwa haki, wala anayeshtaki kwa uaminifu. Mnategemea hoja batili; mnasema uongo. Mnatunga hila na kuzaa uovu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki; hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki. Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo, huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakuna hata mmoja anayedai kwa haki; hakuna hata mmoja anayetetea shauri lake kwa haki. Wanategemea mabishano matupu na kusema uongo, huchukua mimba ya magomvi na kuzaa uovu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakuna anayedai kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hakuna atoaye madai yake kwa haki, wala anayeshtaki kwa uaminifu. Mnategemea hoja batili; mnasema uongo. Mnatunga hila na kuzaa uovu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hakuna amwitaye mwenziwe shaurini kwa kuyataka yaongokayo, wala hakuna ahukumuye kwa kweli, huyakimbilia yaliyo maovyo tu, hujisemea yasiyo maana, huchukua mimba ya maumivu, huzaa mapotovu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hapana adaiye kwa haki, wala hapana atetaye kwa kweli; hutumainia ubatili, hunena uongo; hupata mimba ya madhara, na kuzaa uovu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hakuna anayemushitaki mwenzake kwa haki, wala anayejitetea kwa ukweli. Munategemea mambo ya bure; munasema uongo. Munafanya mipango ya kuleta hasara na kuzaa uovu.