Isaiah 59:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mnaangua mayai ya joka lenye sumu, mnafuma utando wa buibui. Anayekula mayai yenu hufa, na yakipasuliwa nyoka hutokea.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali na kutanda wavu wa buibui. Yeyote alaye mayai yao atakufa, nalo moja likianguliwa, nyoka hutoka humo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mnaangua mayai ya joka lenye sumu, mnafuma utando wa buibui. Anayekula mayai yenu hufa, na yakipasuliwa nyoka hutokea.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali na kutanda wavu wa buibui. Ye yote alaye mayai yao atakufa, na wakati moja lianguliwapo, nyoka mwenye sumu kali hutoka humo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Huangua mayai ya nyoka wenye sumu kali na kutanda wavu wa buibui. Yeyote alaye mayai yao atakufa, na wakati moja lianguliwapo, nyoka hutoka humo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mnaangua mayai ya joka lenye sumu, mnafuma utando wa buibui. Anayekula mayai yenu hufa, na yakipasuliwa nyoka hutokea.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huangua mayai ya pili, hufuma matandabui; mtu akiyala mayai yao hufa, nalo lipasukalo hutoka nyoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Huangua mayai ya fira, na kusuka wavu wa buibui; yeye alaye mayai yao hufa, na hilo livunjwalo hutoka nyoka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Munatoa mayai ya nyoka yenye sumu, munafuma wavu wa buibui. Anayekula mayai yenu anakufa, na yakipasuliwa, nyoka anatokea ndani yake.