Isaiah 59:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mko mbioni kutenda maovu, mnaharakisha kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yenu ni mawazo ya uovu, popote mwendapo mnaacha ukiwa na uharibifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yao ni mawazo maovu; uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mko mbioni kutenda maovu, mnaharakisha kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yenu ni mawazo ya uovu, popote mwendapo mnaacha ukiwa na uharibifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yao ni mawazo mabaya; uharibifu na maangamizi huweka alama njia zao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miguu yao hukimbilia kwenye dhambi, ni myepesi kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yao ni mawazo maovu; uharibifu na maangamizi huonekana katika njia zao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia zao kuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mko mbioni kutenda maovu, mnaharakisha kumwaga damu isiyo na hatia. Mawazo yenu ni mawazo ya uovu, popote mwendapo mnaacha ukiwa na uharibifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Miguu yao hukimbilia mabaya, hupiga mbio kuja kumwaga damu zao wasiokosa, mawazo yao ni mawazo mapotovu, maangamizo na mavunjiko huzijulisha njia zao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Miguu yao hukimbilia mabaya, nao hufanya haraka kumwaga damu isiyo na hatia; mawazo yao ni mawazo ya uovu; ukiwa na uharibifu zaonekana katika njia kuu zao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muko mbio kutenda maovu, muko wepesi kumwanga damu isiyokuwa na kosa. Mawazo yenu ni mawazo ya uovu, popote munapokwenda munaacha ukiwa na uharibifu.