Isaiah 59:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ndio maana haki iko mbali nasi, maongozi ya uadilifu hayapo kwetu. Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu, twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo uadilifu uko mbali nasi, nayo haki haitufikii. Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza, tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza nene.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo hukumu ya haki i mbali nasi, wala haki haitufikilii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ndio maana haki iko mbali nasi, maongozi ya uadilifu hayapo kwetu. Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu, twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo uadilifu uko mbali nasi, nayo haki haitufikii. Tunatazamia nuru, kumbe! yote ni giza, tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo uadilifu uko mbali nasi, nayo haki haitufikii. Tunatazamia nuru, kumbe! Yote ni giza, tunatazamia mwanga, lakini tunatembea katika giza kuu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo hukumu ya haki iko mbali nasi, wala haki haitufikii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ndio maana haki iko mbali nasi, maongozi ya uadilifu hayapo kwetu. Tunatazamia kupata mwanga kumbe ni giza tupu, twatazamia mwangaza, lakini twatembea gizani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hii maamuzi yapasayo yametukalia mbali, nayo yaongokayo hayafiki kwetu. Tukangojea, kuche, lakini tunaona giza tu, tukangojea, kupambazuke, lakini vivyo hivyo tunajiendea na weusi wa usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo hukumu ya haki i mbali nasi, wala haki haitufikilii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, kufuata sheria ya Mungu kuko mbali nasi, haki haifiki kwetu. Tulitazamia kupata mwangaza, kumbe ni giza tupu; tulingojea mwangaza, lakini tunatembea katika giza.