Isaiah 6:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha akaniambia, “Zipumbaze akili za watu hawa, masikio yao yasisikie, macho yao yasione; ili wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa akili zao, na kunigeukia, nao wakaponywa.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu, fanya masikio yao yasisikie, na upofushe macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, nao wakageuka, wakaponywa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha akaniambia, “Zipumbaze akili za watu hawa, masikio yao yasisikie, macho yao yasione; ili wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa akili zao, na kunigeukia, nao wakaponywa.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu, fanya masikio yao yasisikie na upofushe macho yao. Ama sivyo wanaweza kuona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakatambua kwa mioyo yao, nao wakageuka na kuponywa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Fanya mioyo ya watu hawa kuwa migumu, fanya masikio yao yasisikie, na upofushe macho yao. Wasije wakaona kwa macho yao, na wakasikiliza kwa masikio yao, wakaelewa kwa mioyo yao, nao wakageuka, nikawaponywa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Zifanye akili za watu hawa zipumbae, na uyatie uzito masikio yao, na uyafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha akaniambia, “Zipumbaze akili za watu hawa, masikio yao yasisikie, macho yao yasione; ili wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa akili zao, na kunigeukia, nao wakaponywa.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mioyo yao walio ukoo huu uishupaze, nayo masikio yao uyazibe, nayo macho yao uyafumbe, wasije wakaona kwa macho yao, au wakasikia kwa masikio yao, au wakajua maana kwa mioyo yao, wakanigeukia, nikawaponya!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uunoneshe moyo wa watu hawa, ukayatie uzito masikio yao, ukayafumbe macho yao; wasije wakaona kwa macho yao, na kusikia kwa masikio yao, na kufahamu kwa mioyo yao, na kurejea na kuponywa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha akaniambia: Ufanye akili za watu hawa kuwa ngumu, masikio yao yasisikie, macho yao yasione; wasipate kuona kwa macho yao, wasipate kusikia kwa masikio yao, wasipate kuelewa kwa akili zao, na kunigeukia, nao wapate kupona.