Isaiah 6:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hata wakibaki watu asilimia kumi, nao pia watateketezwa. Hao watakuwa kama mvinje au mwaloni ambao kisiki chake kimebaki baada ya kukatwa.” (Kisiki hicho ni mbegu takatifu ya chanzo kipya.)
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi, itaharibiwa tena. Lakini kama vile mvinje au mwaloni ubakizavyo visiki unapokatwa, ndivyo mbegu takatifu itakavyokuwa kisiki katika nchi.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hata wakibaki watu asilimia kumi, nao pia watateketezwa. Hao watakuwa kama mvinje au mwaloni ambao kisiki chake kimebaki baada ya kukatwa.” (Kisiki hicho ni mbegu takatifu ya chanzo kipya.)
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi, itaharibiwa tena. Lakini kama vile mvinje na mwaloni ibakizavyo visiki inapokatwa, ndivyo mbegu takatifu itakavyokuwa kisiki katika nchi.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata kama sehemu ya kumi ya watu watabaki katika nchi, itaharibiwa tena. Lakini kama vile mvinje na mwaloni ibakizavyo visiki inapokatwa, ndivyo mbegu takatifu itakavyokuwa kisiki katika nchi.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hata wakibaki watu asilimia kumi, nao pia watateketezwa. Hao watakuwa kama mvinje au mwaloni ambao kisiki chake kimebaki baada ya kukatwa.” (Kisiki hicho ni mbegu takatifu ya chanzo kipya.)
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tena kama sao litakuwa fungu la kumi tu, litaangamizwa mara nyingine. Litakuwa kama mkwaju au mtamba: ukikatwa, kunasalia shina lake; hilo shina lake litakuwa mbegu takatifu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ijapokuwa imebaki sehemu moja katika sehemu kumi ndani yake, italiwa hii nayo; kama mvinje na kama mwaloni, ambao shina lake limebaki, ingawa imekatwa; kadhalika mbegu takatifu ndiyo shina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hata kukibaki sehemu moja ya kumi ya watu, nao vilevile watateketezwa. Hao watakuwa kama muti wa muvinje au wa mwalo ambao shina lake limebaki kisha kukatwa. Shina hilo ni mbegu takatifu ya mwanzo mupya.