Isaiah 60:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wa wale waliokudhulumu, watakuja na kukuinamia kwa heshima. Wote wale waliokudharau, watasujudu mbele ya miguu yako. Watakuita: ‘Mji wa Mwenyezi-Mungu’, ‘Siyoni, Mji wa Mtakatifu wa Israeli’.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wana wa wale waliokutesa watakuja wakisujudu mbele yako; wote wanaokudharau watasujudu miguuni pako; nao watakuita Mji wa Mwenyezi Mungu, Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa Bwana, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wa wale waliokudhulumu, watakuja na kukuinamia kwa heshima. Wote wale waliokudharau, watasujudu mbele ya miguu yako. Watakuita: ‘Mji wa Mwenyezi-Mungu’, ‘Siyoni, Mji wa Mtakatifu wa Israeli’.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako, wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako nao watakuita Mji wa BWANA, Sayuni wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wana wa wale waliokuonea watakuja wakisujudu mbele yako, wote wanaokudharau watasujudu kwenye miguu yako, nao watakuita Mji wa bwana, Sayuni ya Aliye Mtakatifu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha katika nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wa wale waliokudhulumu, watakuja na kukuinamia kwa heshima. Wote wale waliokudharau, watasujudu mbele ya miguu yako. Watakuita: ‘Mji wa Mwenyezi-Mungu’, ‘Siyoni, Mji wa Mtakatifu wa Israeli’.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao wana wao waliokutesa watakuja kwako na kuinama chini, nao wote waliokutukana watakuangukia penye nyayo za miguu yako, watakuita mji wa Bwana, Sioni wa Mtakatifu wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na wana wa watu wale waliokutesa Watakuja kwako na kukuinamia; Nao wote waliokudharau Watajiinamisha hata nyayo za miguu yako; Nao watakuita, Mji wa BWANA, Sayuni wa Mtakatifu wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wa wale waliokutesa, watakuja na kuinama uso mpaka chini mbele yako. Wote wale waliokuzarau, watapiga magoti kwenye miguu yako. Watakuita: “Muji wa Yawe”, “Sayuni”, “Muji wa Mutakatifu wa Israeli”.