Isaiah 60:7 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Makundi ya kondoo wa Kedari yatakusanywa kwako, utaweza kuwatumia kondoo madume wa Nebayothi kuwa kafara; utawatoa kuwa tambiko inayokubalika madhabahuni pa Mungu, naye ataitukuza nyumba yake tukufu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia, watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu, nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Makundi ya kondoo wa Kedari yatakusanywa kwako, utaweza kuwatumia kondoo madume wa Nebayothi kuwa kafara; utawatoa kuwa tambiko inayokubalika madhabahuni pa Mungu, naye ataitukuza nyumba yake tukufu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia, watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu, nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia, watakubalika kama sadaka juu ya madhabahu yangu, nami nitalipamba Hekalu langu tukufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo dume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Makundi ya kondoo wa Kedari yatakusanywa kwako, utaweza kuwatumia kondoo madume wa Nebayothi kuwa kafara; utawatoa kuwa tambiko inayokubalika madhabahuni pa Mungu, naye ataitukuza nyumba yake tukufu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makundi yote ya Kedari, yale ya mbuzi na ya kondoo yatakusanyika kwako, madume ya Nebayoti utayatumia ya tambiko, yatanipendeza juu ya meza ya kunitambikia; ndivyo, nitakavyoitukuza Nyumba ya utukufu wangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Makundi yote ya Kedari yatakusanyika kwako, Kondoo waume wa Nebayothi watakutumikia; Watapanda juu ya madhabahu yangu kwa kibali, Nami nitaitukuza nyumba ya utukufu wangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Makundi ya nyama wa inchi ya Kedari yatakusanyika kwako, utaweza kuwatumia kondoo dume wa Nebayoti; utatoa sadaka inayokubaliwa kwenye mazabahu ya Mungu, naye ataitukuza nyumba yake tukufu.