Isaiah 60:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hakika visiwa vinanitazama; merikebu za Tarshishi ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la Bwana, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hakika visiwa vinanitazama, merikebu za Tarshishi ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya BWANA, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hakika visiwa vinanitazama, merikebu za Tarshishi ndizo zinazotangulia, zikiwaleta wana wenu kutoka mbali, wakiwa na fedha na dhahabu zao, kwa heshima ya bwana, Mungu wenu, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli, kwa maana amekujalia utukufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ni meli zitokazo nchi za mbali, zikitanguliwa na meli za Tarshishi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na fedha na dhahabu yao, kwa sifa ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mtukufu wa Israeli, maana amewafanya mtukuke.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani visiwa vinaningojea, nazo merikebu za Tarsisi zitakuwa za kwanza za kuwaleta wanao toka nchi za mbali; fedha zao na dhahabu zao wanazo za kulitolea Jina la Bwana Mungu wako, kwa kuwa yeye aliye Mtakatifu wa Isiraeli amekupa utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakika yake visiwa vitaningojea, Na merikebu za Tarshishi kwanza, Ili kuleta wana wako kutoka mbali, Na fedha yao na dhahabu yao pamoja nao, Kwa ajili ya jina la BWANA, Mungu wako, Kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli, Kwa kuwa amekutukuza wewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ni mashua zinazotoka katika inchi za mbali, zikitanguliwa na mashua za Tarsisi. Zinawaleta watoto wako, pamoja na feza na zahabu yao, kwa sifa ya Yawe, Mungu wako, kwa sifa ya Mungu, Mutukufu wa Israeli, maana amewafanya mupate utukufu.