Isaiah 61:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivika vazi la wokovu, amenivalisha vazi la uadilifu, kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua, kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ninafurahia sana katika Mwenyezi Mungu, nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu. Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu, na kunipamba kwa joho la haki, kama vile bwana arusi apambavyo kichwa chake kama kuhani, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vito vyake vya thamani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivika vazi la wokovu, amenivalisha vazi la uadilifu, kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua, kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ninafurahia sana katika BWANA, nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu. Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu na kunipamba kwa joho la haki, kama vile bwana arusi apambavyo kichwa chake kama kuhani, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vito vyake vya thamani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ninafurahia sana katika bwana, nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu. Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu, na kunipamba kwa joho la haki, kama vile bwana arusi apambavyo kichwa chake kama kuhani, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vito vyake vya thamani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana harusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi harusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitafurahi sana kwa sababu ya Mwenyezi-Mungu, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivika vazi la wokovu, amenivalisha vazi la uadilifu, kama bwana arusi ajipambavyo kwa shada la maua, kama bibi arusi ajipambavyo kwa johari zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kufurahi nitamfurahia Bwana, roho yangu itampigia Mungu wangu shangwe, kwani amenivika mavazi ya wokovu, akanifunika kwa kanzu ya wongofu, niwe kama mchumba mume, akiutengeneza urembo wa kichwani kuwa kama wa mtambikaji, au kama mchumba mke, akijipamba na kuvaa vito vyake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitafurahi sana kwa sababu ya Yawe, nafsi yangu itashangilia kwa sababu ya Mungu wangu. Maana amenivalisha nguo ya wokovu, amenifunika kanzu ya haki, kama bwana arusi anavyojipamba kwa shada la maua, kama bibi arusi anavyojipamba kwa ushanga wake.