Isaiah 61:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya moyo mzito. Nao wataitwa mialoni madhubuti, aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, ili kuwapa taji za uzuri badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. Nao wataitwa mialoni ya haki, pando la Mwenyezi Mungu, ili kuonesha utukufu wake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na Bwana, ili atukuzwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya moyo mzito. Nao wataitwa mialoni madhubuti, aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. Nao wataitwa mialoni ya haki, pando la BWANA kwa ajili ya kuonyesha utukufu wake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
na kuwapa mahitaji wale wanaohuzunika katika Sayuni, ili kuwapa taji ya uzuri badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho ya kukata tamaa. Nao wataitwa mialoni ya haki, pando la bwana, ili kuonyesha utukufu wake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
niwape wale wanaoomboleza katika Siyoni taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya moyo mzito. Nao wataitwa mialoni madhubuti, aliyopanda Mwenyezi-Mungu kuonesha utukufu wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
niwapoze mioyo yao wausikitikiao Sioni, nikiwapa vilemba penye majivu na mafuta ya furaha penye mavazi ya matanga na mashangilio penye roho za kuzimia, watu wawaite Mivule iongokayo na Shamba la Bwana la kujipatia matukuzo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji ya maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kuwapa wale wanaoomboleza katika Sayuni taji la maua pahali pa majivu juu ya kichwa, mafuta ya kuangarisha kwa furaha pahali pa maombolezo, nguo ya sifa pahali pa moyo muzito. Nao wataitwa miti ya mialo ya haki, Yawe aliyopanda kuonyesha utukufu wake.