Isaiah 61:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa vile mlipata aibu maradufu, watu wakaona kuwa fedheha ni majaliwa yenu, sasa mtapata eneo maradufu kuwa mali yenu, na furaha yenu itadumu milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Badala ya aibu yao watu wangu watapokea sehemu maradufu, na badala ya fedheha watafurahia katika urithi wao; hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao, nayo furaha ya milele itakuwa yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa vile mlipata aibu maradufu, watu wakaona kuwa fedheha ni majaliwa yenu, sasa mtapata eneo maradufu kuwa mali yenu, na furaha yenu itadumu milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Badala ya aibu yao watu wangu watapokea sehemu maradufu, na badala ya fedheha watafurahia katika urithi wao; hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao, nayo furaha ya milele itakuwa yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Badala ya aibu yao watu wangu watapokea sehemu maradufu, na badala ya fedheha watafurahia katika urithi wao; hivyo watarithi sehemu maradufu katika nchi yao, nayo furaha ya milele itakuwa yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa vile mlipata aibu maradufu, watu wakaona kuwa fedheha ni majaliwa yenu, sasa mtapata eneo maradufu kuwa mali yenu, na furaha yenu itadumu milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Penye soni walizotiwa watapata malipo mara mbili, penye matusi watalishangilia fungu lao. Kweli katika nchi yao watakuwa wenye mafungu mawili, tena watapata kuchangamka kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Badala ya aibu yenu mtapata maradufu, na badala ya fedheha wataifurahia sehemu yao; basi katika nchi yao watamiliki maradufu; furaha yao itakuwa ya milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa vile mulipata haya mara mbili, watu wakaona kwamba mazarau ni majaliwa yenu, sasa mutapata sehemu mara mbili kuwa mali yenu, na furaha yenu itadumu milele.