Isaiah 61:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyanganyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Kwa maana Mimi, Mwenyezi Mungu, napenda haki, na ninachukia unyang’anyi na uovu. Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao na kufanya agano la milele nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana mimi, Bwana, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyang'anyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Kwa maana Mimi, BWANA, napenda haki, ninachukia unyang'anyi na uovu. Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao ya haki na kufanya Agano la milele nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Kwa maana Mimi, bwana, napenda haki, na ninachukia unyang’anyi na uovu. Katika uaminifu wangu nitawapa malipo yao na kufanya agano la milele nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wizi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyanganyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mimi Bwana ninapenda maamuzi yapasayo, nikachukiwa nayo yaliyopokonywa kwa upotovu, kwa hiyo nitawapa kwa kweli yayapasayo matendo yao, nitafanya nao agano la kale na kale.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana mimi, BWANA, naipenda hukumu ya haki, nauchukia wivi na uovu; nami nitawalipa malipo katika kweli, nitaagana nao agano la milele.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mimi Yawe ninapenda watu wafuate sheria yangu; ninachukia unyanganyi na uovu. Nitawatunza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.