Isaiah 61:9 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa; watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine. Kila atakayewaona atakiri kwamba wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, na uzao wao miongoni mwa makabila ya watu. Wale wote watakaowaona watatambua kuwa ni taifa ambalo Mwenyezi Mungu amelibariki.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa; watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine. Kila atakayewaona atakiri kwamba wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa na uzao wao miongoni mwa kabila za watu. Wale wote watakaowaona watatambua kuwa ni taifa ambalo BWANA amelibariki.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wazao wao watajulikana miongoni mwa mataifa, na uzao wao miongoni mwa kabila za watu. Wale wote watakaowaona watatambua kuwa ni taifa ambalo bwana amelibariki.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika makabila ya watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wazawa wao watakuwa maarufu kati ya mataifa; watajulikana kuwa maarufu kati ya watu wengine. Kila atakayewaona atakiri kwamba wao ni watu aliowabariki Mwenyezi-Mungu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mazao yao yatajulikana kwa wamizimu, nao waliotoka miilini mwao watajulikana katikati ya makabila ya watu; wote watakaowaona watawatambua, ya kuwa ndio mazao yaliyobarikiwa na Bwana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kizazi chao kitajulikana katika mataifa, na uzao wao katika kabila za watu; wote wawaonao watakiri ya kuwa wao ni kizazi kilichobarikiwa na BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wazao wao watajulikana kati ya mataifa; watajulikana kati ya watu wengine. Kila mutu atakayewaona atakubali kwamba wao ni watu waliobarikiwa na Yawe.