Isaiah 62:8 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia, naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema: “Sitawapa tena maadui zako nafaka yako; wala wageni hawatakunywa tena divai yako ambayo umeitolea jasho.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wake wenye nguvu: “Kamwe sitawapa tena adui zenu nafaka zenu kama chakula chao; kamwe wageni hawatakunywa tena divai mpya ambayo mmeitaabikia,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia, naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema: “Sitawapa tena maadui zako nafaka yako; wala wageni hawatakunywa tena divai yako ambayo umeitolea jasho.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wake wenye nguvu: “Kamwe sitawapa tena adui zenu nafaka zenu kama chakula chao; kamwe wageni hawatakunywa tena divai mpya ambayo hiyo mmeitaabikia,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume na kwa mkono wake wenye nguvu: “Kamwe sitawapa tena adui zenu nafaka zenu kama chakula chao; kamwe wageni hawatakunywa tena divai mpya ambayo mmeitaabikia,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kulia, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu ameapa kwa mkono wake wa kulia, naam, ameapa kwa mkono wake wenye nguvu akisema: “Sitawapa tena maadui zako nafaka yako; wala wageni hawatakunywa tena divai yako ambayo umeitolea jasho.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana ameapa na kuutaja mkono wake wa kuume ulio na nguvu kwamba: Sitazitoa tena ngano zako, ziliwe na adui zako, wala wana wa nchi ngeni wasinywe tena pombe zako, ulizozisumbukia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
BWANA ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe ameapa kwa uwezo wake mukubwa, ameapa kwa nguvu yake akisema: Sitawapa tena waadui zako ngano yako; wala wageni hawatakunywa tena divai yako ambayo umeitoshea jasho.