Isaiah 62:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo, mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu. Nyinyi mliochuma zabibu hizo, mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
lakini wale waivunao nafaka wataila na kumsifu Mwenyezi Mungu, nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake katika nyua za patakatifu pangu.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo, mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu. Nyinyi mliochuma zabibu hizo, mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
lakini wale waivunao nafaka wataila na kumsifu BWANA, nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake katika nyua za patakatifu pangu.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
lakini wale waivunao nafaka wataila na kumsifu bwana, nao wale wakusanyao zabibu watainywa divai yake katika nyua za patakatifu pangu.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bali nyinyi mliyoivuna nafaka hiyo, mtaila na kunitukuza mimi Mwenyezi-Mungu. Nyinyi mliochuma zabibu hizo, mtakunywa divai yake katika nyua zangu takatifu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila watakaozivuna ndio watakaozila, wamshukuru Bwana, nao watakaozichuma ndio watakaozinywa nyuani penye Patakatifu pangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi BWANA; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini ninyi muliovuna ngano hiyo, mutaikula na kunitukuza mimi Yawe. Ninyi muliochuma mizabibu hiyo, mutakunywa divai yake katika viwanja vya hekalu langu takatifu.