Isaiah 63:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ng'ombe wapelekwavyo malishoni bondeni, ndivyo roho ya Mungu ilivyowapumzisha watu wake. Ndivyo ee Mungu ulivyowaongoza watu wako, nawe ukajipatia jina tukufu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kama ng’ombe wanaoshuka bondeni, walipewa pumziko na Roho wa Mwenyezi Mungu. Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako ili kujipatia jina tukufu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama ng'ombe washukao bondeni, Roho ya Bwana akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ng'ombe wapelekwavyo malishoni bondeni, ndivyo roho ya Mungu ilivyowapumzisha watu wake. Ndivyo ee Mungu ulivyowaongoza watu wako, nawe ukajipatia jina tukufu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kama ng'ombe washukao bondeni kwenye malisho, walipewa pumziko na Roho wa BWANA. Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kama ng’ombe washukao bondeni kwenye malisho, walipewa pumziko na Roho wa bwana. Hivi ndivyo ulivyowaongoza watu wako ili kujipatia mwenyewe jina tukufu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama ng'ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA ikawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ng'ombe wapelekwavyo malishoni bondeni, ndivyo roho ya Mungu ilivyowapumzisha watu wake. Ndivyo ee Mungu ulivyowaongoza watu wako, nawe ukajipatia jina tukufu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama kundi linavyotelemka bondeni, ndivyo, roho ya Bwana ilivyowapeleka pa kupumzikia. Hivyo ndivyo, ulivyowaongoza walio ukoo wako, ujipatie Jina lenye utukufu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA akawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama vile ngombe wanavyopelekwa kwa kulishwa katika bonde, ndivyo Roho wa Mungu alivyowapumzisha watu wake. Ndivyo, ee Mungu ulivyowaongoza watu wako, nawe ukajipatia jina tukufu.