Isaiah 63:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ututazame kutoka mbinguni ee Mungu, uone, utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu. Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako? Usiache kutuonesha upendo wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama chini kutoka mbinguni ukaone kutoka kiti chako cha enzi kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu. Uko wapi wivu wako na uweza wako? Umetuzuilia wema wako na huruma zako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ututazame kutoka mbinguni ee Mungu, uone, utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu. Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako? Usiache kutuonesha upendo wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama chini kutoka mbinguni ukaone kutoka katika kiti chako cha enzi kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu. Uko wapi wivu wako na uweza wako? Umetuzuilia wema wako na huruma zako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama chini kutoka mbinguni ukaone kutoka kiti chako cha enzi kilichoinuliwa juu, kitakatifu na kitukufu. Uko wapi wivu wako na uweza wako? Umetuzuilia wema wako na huruma zako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ututazame kutoka mbinguni ee Mungu, uone, utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu. Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako? Usiache kutuonesha upendo wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Chungulia toka mbinguni! Tazama toka Kao lako takatifu lenye utukufu! Wivu wako uko wapi? Matendo yako ya nguvu yako wapi? Huruma zako zinazovuma moyoni mwako zimejizuia, zisifike kwangu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Utuchungulie kutoka mbinguni, ee Mungu, uone, utuangalie kutoka makao yako matakatifu na matukufu. Iko wapi bidii yako kwa ajili yetu na nguvu yako? Hatuoni tena upendo na huruma yako.