Isaiah 63:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana wewe ndiwe Baba yetu; Abrahamu, mzee wetu, hatujali, naye Israeli hatutambui; lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ni Baba yetu. Wewe umeitwa tangu kale: “Mkombozi wetu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini wewe ni Baba yetu, ingawa Ibrahimu hatufahamu sisi wala Israeli hatutambui; wewe, Ee Mwenyezi Mungu, ndiwe Baba yetu, Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, Bwana, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana wewe ndiwe Baba yetu; Abrahamu, mzee wetu, hatujali, naye Israeli hatutambui; lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ni Baba yetu. Wewe umeitwa tangu kale: “Mkombozi wetu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini wewe ni Baba yetu, ingawa Abrahamu hatufahamu sisi wala Israeli hatutambui; wewe, Ee BWANA, ni Baba yetu, Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini wewe ni Baba yetu, ingawa Ibrahimu hatufahamu sisi wala Israeli hatutambui; wewe, Ee bwana, ndiwe Baba yetu, Mkombozi wetu tangu zamani za kale ndilo jina lako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana wewe ndiwe Baba yetu; Abrahamu, mzee wetu, hatujali, naye Israeli hatutambui; lakini wewe, ee Mwenyezi-Mungu, ni Baba yetu. Wewe umeitwa tangu kale: “Mkombozi wetu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani wewe ndiwe baba yetu; kwani Aburahamu hakutujua, wala Isiraeli hakututambua. Wewe Bwana ndiwe baba yetu; Mkombozi wetu ndilo jina lako la kale.*
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Ibrahimu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana wewe ndiwe Baba yetu; Abrahamu, babu yetu, hatujali, naye Israeli hatutambui; lakini wewe, ee Yawe, ni Baba yetu. Wewe umeitwa tangu zamani: Mukombozi wetu.