Isaiah 63:17 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu, mbona unatukosesha njia zako? Mbona unatufanya kuwa wakaidi hata tusikuogope? Rudi ee Mungu kwa ajili ya watumishi wako, makabila ambayo daima yalikuwa mali yako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako, na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? Rudi kwa ajili ya watumishi wako, yale makabila ambayo ni urithi wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu, mbona unatukosesha njia zako? Mbona unatufanya kuwa wakaidi hata tusikuogope? Rudi ee Mungu kwa ajili ya watumishi wako, makabila ambayo daima yalikuwa mali yako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, kwa nini unatuacha tuende mbali na njia zako na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? Rudi kwa ajili ya watumishi wako, yale makabila ambayo ni urithi wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana, kwa nini unatuacha twende mbali na njia zako, na kuifanya mioyo yetu migumu hata hatukukuheshimu? Rudi kwa ajili ya watumishi wako, yale makabila ambayo ni urithi wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu, mbona unatukosesha njia zako? Mbona unatufanya kuwa wakaidi hata tusikuogope? Rudi ee Mungu kwa ajili ya watumishi wako, makabila ambayo daima yalikuwa mali yako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mbona umetupoteza, Bwana, tukaziacha njia zako? Mbona umeishupaza mioyo yetu, isikuogope? Rudi kwa ajili ya watumishi wako walio milango ya fungu lako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanyiza kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, kabila za urithi wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, mbona unatukosesha njia zako? Mbona unaifanya mioyo yetu kuwa migumu hata tusikuogope? Urudie, ee Mungu, kwa ajili ya watumishi wako, makabila ambayo yalikuwa mali yako siku zote.