Isaiah 63:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Naam, nimekamua zabibu peke yangu, wala hakuna mtu aliyekuja kunisaidia. Nimeyakanyaga mataifa kwa hasira yangu, niliyapondaponda kwa ghadhabu yangu. Nguo zangu zimejaa madoa ya damu yao, imeyachafua kabisa mavazi yangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nimekanyaga shinikizo la kukamulia zabibu peke yangu; kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, na kutia madoa nguo zangu zote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Naam, nimekamua zabibu peke yangu, wala hakuna mtu aliyekuja kunisaidia. Nimeyakanyaga mataifa kwa hasira yangu, niliyapondaponda kwa ghadhabu yangu. Nguo zangu zimejaa madoa ya damu yao, imeyachafua kabisa mavazi yangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; kutoka katika mataifa hakuna mtu awaye yote aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda mataifa kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone matone kwenye mavazi yangu na kutia madoa nguo zangu zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nimekanyaga shinikizo la zabibu peke yangu; kutoka mataifa hakuna mtu aliyekuwa pamoja nami. Nimewaponda kwa miguu katika hasira yangu na kuwakanyaga chini katika ghadhabu yangu; damu yao ilitia matone kwenye mavazi yangu, na kutia madoa nguo zangu zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, niliwakanyaga kwa hasira yangu, Niliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Naam, nimekamua zabibu peke yangu, wala hakuna mtu aliyekuja kunisaidia. Nimeyakanyaga mataifa kwa hasira yangu, niliyapondaponda kwa ghadhabu yangu. Nguo zangu zimejaa madoa ya damu yao, imeyachafua kabisa mavazi yangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kweli nimekamua kamulioni mimi peke yangu, pasipokuwa na mtu mwingine, nikawakamua kwa makali yangu, nikawaponda kwa moto wa machafuko yangu, damu zao zikazirukia nguo zangu, nikayachafua mavazi yangu yote,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nalikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, naliwakanyaga kwa hasira yangu, Naliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kweli, nimekamua mizabibu peke yangu, wala hakuna mutu aliyekuja kunisaidia. Nimeyakanyaga mataifa kwa hasira yangu, niliyapondaponda kwa kasirani yangu. Nguo zangu zimejaa madoa ya damu yao, imechafua kabisa nguo yangu.