Isaiah 63:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nilitazama na hapakuwa na wa kunisaidia; nilishangaa hapakuwa na wa kuniunga mkono. Lakini nilijipatia ushindi kwa mkono wangu, ghadhabu yangu ilinihimiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nilitazama, lakini hapakuwa yeyote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hapakuwa yeyote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nilitazama na hapakuwa na wa kunisaidia; nilishangaa hapakuwa na wa kuniunga mkono. Lakini nilijipatia ushindi kwa mkono wangu, ghadhabu yangu ilinihimiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nilitazama, lakini hakuwepo ye yote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hakuwepo ye yote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nilitazama, lakini hakuwepo yeyote wa kunisaidia, nilishangaa kwa kuwa hakuwepo yeyote aliyetoa msaada; hivyo mkono wangu wenyewe ndio ulionifanyia wokovu, na ghadhabu yangu mwenyewe ndiyo iliyonitegemeza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nikatazama, wala hapakuwa na wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nilitazama na hapakuwa na wa kunisaidia; nilishangaa hapakuwa na wa kuniunga mkono. Lakini nilijipatia ushindi kwa mkono wangu, ghadhabu yangu ilinihimiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nikatazama, lakini hakuna msaidiaji, nikachungulia na kushangaa, lakini hakuna ashikizaye; ndipo, mkono wangu uliponitumikia kuwa wa kuokoa, nao moto wa machafuko yangu ukanishikiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nikatazama, wala hakuna wa kusaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Niliangalia, hapakukuwa wa kunisaidia; nilishangaa, hapakukuwa wa kuniunga mukono. Lakini nilijipatia ushindi kwa mukono wangu, kasirani yangu ilinisaidia.