Isaiah 63:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nitasimulia kuhusu wema wa Mwenyezi Mungu, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo Mwenyezi Mungu ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nitautaja wema wa Bwana, sifa za Bwana kwa yote aliyotukirimia Bwana; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nitasimulia juu ya wema wa BWANA, kwa ajili ya matendo ambayo kwayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo BWANA ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nitasimulia juu ya wema wa bwana, kwa matendo ambayo apaswa kusifiwa, sawasawa na yote ambayo bwana ametenda kwa ajili yetu: naam, mambo mengi mema aliyoyatenda kwa ajili ya nyumba ya Israeli, sawasawa na huruma zake na wema wake mwingi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitasimulia fadhili za Mwenyezi-Mungu; nitataja matendo yake yote yastahiliyo sifa, kwa sababu ya yote aliyotutendea, wema wake mkuu aliowapa Waisraeli kwa huruma yake, kadiri ya wingi wa fadhili zake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
*Nitawakumbusha magawio ya Bwana na kumtukuza Bwana kwa ajili yao yote, aliyotutendea Bwana; mema yake ni mengi, aliyoutendea mlango wa Isiraeli kwa huruma zake aliwagawia mengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitakumbusha mema ya Yawe, sifa za Yawe, matendo yake yote kwetu, mambo mazuri aliyowatendea Waisraeli, rehema yake, na wingi wa wema wake.