Isaiah 65:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini nitafanya nini na nyinyi mnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu, msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu, nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’, na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’?
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Bali ninyi mnaomwacha Mwenyezi Mungu na kuusahau mlima wangu mtakatifu, ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa kwa ajili ya Ajali,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Bali ninyi mmwachao Bwana, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandika meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini nitafanya nini na nyinyi mnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu, msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu, nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’, na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’?
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Bali kwenu ninyi mnaomwacha BWANA na kuusahau mlima wangu mtakatifu, ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa kwa ajili ya Ajali,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Bali kwenu ninyi mnaomwacha bwana na kuusahau mlima wangu mtakatifu, ninyi mnaoandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kujaza mabakuli ya mvinyo uliochanganywa kwa ajili ya Ajali,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Bali ninyi mmwachao BWANA, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandaa meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini nitafanya nini na nyinyi mnaoniacha mimi Mwenyezi-Mungu, msioujali Siyoni, mlima wangu mtakatifu, nyinyi mnaoabudu mungu ‘Gadi’, na kumtolea tambiko ya divai mungu ‘Meni’?
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ninyi mliomwacha Bwana, mkausahau mlima wangu mtakatifu, mkamtandikia meza Mwenye kura, naye Mwenye maaguo mkammiminia vinyweo vilivyojaa mvinyo za tambiko,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Bali ninyi mmwachao BWANA, na kuusahau mlima wangu mtakatifu, na kuandika meza kwa ajili ya Bahati, na kuijazia Ajali vyombo vya divai iliyochanganyika;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini nitafanya nini na ninyi munaoniacha mimi Yawe, musioujali Sayuni, mulima wangu mutakatifu, munaotolea miungu chakula na divai kusudi iwapatie bahati zuri.