Isaiah 65:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na Mwenyezi Mungu, wao na wazao wao pamoja nao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na Bwana, na watoto wao pamoja nao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hawatajitaabisha kwa kazi bure wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na BWANA, wao na wazao wao pamoja nao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa watoto ili wapatwe na majanga, kwa kuwa watakuwa taifa lililobarikiwa na bwana, wao na wazao wao pamoja nao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto wa kupata maafa; maana watakuwa waliobarikiwa na Mwenyezi-Mungu, wamebarikiwa wao pamoja na wazawa wao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hawatasumbuka bure, wala hawatazaa watoto watakaogunduliwa na kifo, kwani watakuwa mazao yaliyobarikiwa na Bwana, wao wenyewe nao watakaotoka miilini mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hawatajitaabisha kwa kazi bure, wala hawatazaa kwa taabu; kwa sababu wao ni wazao wa hao waliobarikiwa na BWANA, na watoto wao pamoja nao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kazi zao hazitakuwa bure, wala hawatazaa watoto watakaopatwa na musiba; maana watakuwa waliobarikiwa na Yawe, wamebarikiwa wao pamoja na wazao wao.