Isaiah 65:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yao wayalipie na maovu ya wazee wao. Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani, wakanitukana mimi huko vilimani. Nitawafanya walipe kwa wingi, watayalipia matendo yao ya awali.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
dhambi zenu na dhambi za baba zenu,” asema Mwenyezi Mungu. “Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima na kunichokoza mimi juu ya vilima, nitawapimia mapajani mwao malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema Bwana, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yao wayalipie na maovu ya wazee wao. Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani, wakanitukana mimi huko vilimani. Nitawafanya walipe kwa wingi, watayalipia matendo yao ya awali.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
dhambi zenu na dhambi za baba zenu,” asema BWANA. “Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima na kunichokoza mimi juu ya vilima, nitawapimia mapajani mwao malipo makamilifu kwa ajili ya matendo yao ya zamani.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
dhambi zenu na dhambi za baba zenu,” asema bwana. “Kwa sababu walitoa dhabihu za kuteketezwa juu ya milima na kunichokoza mimi juu ya vilima, nitawapimia mapajani mwao malipo makamilifu kwa matendo yao ya zamani.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mimi Mwenyezi-Mungu, nitawalipiza maovu yao wayalipie na maovu ya wazee wao. Wao waliifukizia ubani miungu yao milimani, wakanitukana mimi huko vilimani. Nitawafanya walipe kwa wingi, watayalipia matendo yao ya awali.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Manza zenu, mlizozikora, pamoja nazo za baba zenu na mzilipe, ndivyo, Bwana anavyosema; maana wamevukiza milimani juu, nako vilimani juu wamenibeua. Nami kwanza nitawapimia malipo ya matendo yao, wayachukue vifuani mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
maovu yenu na maovu ya baba zenu pamoja, asema BWANA, ninyi mliofukiza uvumba juu ya milima, na kunitukana juu ya vilima; basi, kwa ajili ya hayo nitawapimia kwanza kazi yao vifuani mwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawalipiza maovu yao wayalipe vilevile maovu ya babu zao. –Ni Yawe anayesema hivyo.– Wao waliifukizia ubani miungu yao kwenye milima, wakanitukana mimi kule juu ya vilima. Nitawalipa sawa inavyostahili, watayalipa matendo yao ya zamani.