Isaiah 66:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi; mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi. Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu, lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia, nanyi mtastawi kama majani; mkono wa Mwenyezi Mungu utajulikana kwa watumishi wake, bali ghadhabu yake kali itaoneshwa kwa adui zake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa Bwana utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi; mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi. Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu, lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia, nanyi mtastawi kama majani; mkono wa BWANA utajulikana kwa watumishi wake, bali ghadhabu yake kali itaonyeshwa kwa adui zake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati mtakapoona jambo hili, mioyo yenu itashangilia, nanyi mtastawi kama majani; mkono wa bwana utajulikana kwa watumishi wake, bali ghadhabu yake kali itaonyeshwa kwa adui zake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa BWANA utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtayaona hayo na mioyo yenu itafurahi; mifupa yenu itapata nguvu kama majani mabichi. Hapo itajulikana kuwa mimi Mwenyezi-Mungu huwalinda watumishi wangu, lakini nikikasirika huwaadhibu maadui zangu.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtakapoyaona, mioyo yenu itafurahi, nayo mifupa yenu itachipuka kama majani mabichi, nao mkono wake Bwana utajulikana kwa watumishi wake, nayo makali yake yatajulikana kwa adui zake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nanyi mtaona, na mioyo yenu itafurahi, na mifupa yenu itasitawi kama majani mabichi; na mkono wa BWANA utajulikana, uwaelekeao watumishi wake, naye atawaonea adui zake ghadhabu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutayaona hayo na mioyo yenu itafurahi; mifupa yenu itastawi tena kama vile majani mabichi. Kwa hiyo itajulikana kwamba mimi Yawe ninawalinda watumishi wangu, lakini nikikasirika ninawaazibu waadui zangu.