Isaiah 66:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazama, Mwenyezi Mungu anakuja na moto, magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli, atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali, na karipio lake pamoja na miali ya moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana Bwana atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazama, BWANA anakuja na moto, magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli, atatelemsha hasira yake kwa ghadhabu kali na karipio lake pamoja na miali ya moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazama, bwana anakuja na moto, magari yake ya vita ni kama upepo wa kisulisuli, atateremsha hasira yake kwa ghadhabu kali, na karipio lake pamoja na miali ya moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kimbunga. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na onyo lake litekelezwe kwa miali ya moto.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani na mwone, Bwana anavyokuja motoni, magari yake yakikimbizwa na upepo mkali, awalipe kwa moto wa makali yake na kwa mavumo ya moto uwakao na nguvu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atakuja kama moto, na magari yake ya vita ni kama zoruba. Ataiacha hasira yake ifanye kazi yake kwa ukali, na maonyo yake yatimizwe kwa ndimi za moto.