Isaiah 66:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake Mwenyezi Mungu atatekeleza hukumu juu ya watu wote, nao wengi watakuwa ni wale waliouawa na Mwenyezi Mungu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa maana Bwana atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na Bwana watakuwa wengi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake BWANA atatekeleza hukumu juu ya watu wote, nao wengi watakuwa ni wale waliouawa na BWANA.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa maana kwa moto na kwa upanga wake bwana atatekeleza hukumu juu ya watu wote, nao wengi watakuwa ni wale waliouawa na bwana.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa maana BWANA atatoa hukumu kwa watu wote kwa moto, na kwa upanga wake, nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atatoa hukumu kwa moto, atawaadhibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana atawapatiliza wote wenye miili ya kimtu kwa moto na kwa upanga, nao watakaouawa naye Bwana watakuwa wengi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa maana BWANA atateta na wote wenye mwili, kwa moto na kwa upanga wake; nao watakaouawa na BWANA watakuwa wengi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atatoa hukumu kwa moto atawaazibu watu wote kwa upanga; nao atakaowaangamiza watakuwa wengi.