Isaiah 66:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, hadi mlima wangu mtakatifu huko Yerusalemu kama sadaka kwa Mwenyezi Mungu, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema Mwenyezi Mungu. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la Mwenyezi Mungu, katika vyombo vilivyotakaswa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa Bwana, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema Bwana; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa Bwana katika chombo safi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka katika mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema BWANA. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la BWANA, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nao watawaleta ndugu zenu wote, kutoka mataifa yote, mpaka kwenye mlima wangu mtakatifu katika Yerusalemu kama sadaka kwa bwana, juu ya farasi, katika magari ya vita na magari makubwa, juu ya nyumbu na ngamia,” asema bwana. “Watawaleta, kama Waisraeli waletavyo sadaka zao za nafaka, katika Hekalu la bwana, katika vyombo safi kwa kufuata desturi za ibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watawarejesha ndugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Mwenyezi-Mungu. Watawaleta wamepanda farasi, nyumbu, ngamia na magari ya farasi mpaka Yerusalemu, kwenye mlima wangu mtakatifu. Watawaleta kama Waisraeli waletavyo sadaka ya nafaka katika chombo safi hadi nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watawaleta ndugu zenu wote kuwa kipaji cha tambiko cha Bwana wakiwatoa kwenye mataifa yote; nao watapanda farasi na magari, wengine watachukuliwa katika machela, wengine watapanda nyumbu na ngamia, waje kufika Yerusalemu kwenye mlima wangu mtakatifu; ndivyo, Bwana anavyosema. Watawaleta hivyo, kama wana wa Isiraeli wanavyovipeleka vipaji vya tambiko Nyumbani mwa Bwana katika vyombo vilivyotakaswa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watawaleta ndugu zenu wote kutoka mataifa yote, kuwa sadaka kwa BWANA, juu ya farasi, na katika magari, na katika machela, na juu ya nyumbu, na juu ya wanyama wepesi, mpaka mlima wangu mtakatifu Yerusalemu, asema BWANA; kama vile wana wa Israeli waletavyo sadaka yao nyumbani kwa BWANA katika chombo safi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watawarudisha wandugu zenu wote kutoka katika mataifa yote kama matoleo yangu mimi Yawe. Watawaleta juu ya farasi, juu ya nyumbu, juu ya ngamia na ndani ya magari na juu ya vipoyi mpaka Yerusalema, kwenye mulima wangu mutakatifu. Watawaleta kama Waisraeli wanavyoleta sadaka ya unga katika chombo safi mpaka ndani ya nyumba yangu mimi Yawe.